Toleo hili la Tor Browser mpya linalenga kuwasaidia watumiaji kuelewa onion services.

Njia za onio za Tor hubaki kuwa ni njia bora ya kupata mawasiliano yaliyosimbwa katika mtandao. Kwa onion service (. anwani za onion), wasimamizi wa tovuti wanaweza wakawapa watumiaji wao muunganiko usiojulikana ambayo ni metadata huru au metadata iliyofichwa na watu wasiohusika. Pia onion services ni moja kati ya teknolojia ya ukwepaji wa udhibiti chache zinazo waruhusu watumiaji kuperuzi katika udhibiti huku wakilinda faragha na utambulisho wao.

Kwa mara ya kwanza, watumiaji wa Tor Browser wataweza kuchagua kutumia tovuti za onion moja kwa moja popote tovuti zitakapo patikana. Kwa miaka mingi, baadhi ya tovuti haiojulikani imetumia onion services na huduma mbadala, na hii huendelea kuwa chaguo bora. Sasa kuna chaguo kwa tovuti ambazo inawataka watumiaji wake kujua kuhusu onion service kuwaalika kuchagua kutumia anwani zao za onioni.

Mpya ni nini?

Eneo la Onion

Wachapishaji wa tovuti sasa wanaweza wakatangaza onion service zao kwenye watumiaji wa Tor kwa kuongeza HTTP header. Unapotembelea tovuti ambazo zina anwani za onion na onion location zilizowezeshwa kupitia Tor Browser, watumiaji wata hamasishwa kuhusu toleo la onion service la tovuti na wataulizwa kuchagua kuboresha onion service katika utumiaji wao wa kwanza.

Tor Browser 9.5 Eneo la Onion]


Kama wewe ni mtengenezaji programu, jifunze jinsi ya kuwezesha onion location kwenye onion service zako.


Uthibitisho wa onion

Wasimamizi wa onion services ambao hutaka kuongeza safu ya ziada ya ulinzi katika toviti sasa wanaweza wakaweza jozi ya funguo kupata umiliki na uthibitisho.

Tor Browser 9.5 Uthibitisho wa Onion]

Watumiaji wa Tor Browser wanaweza kutunza fuguo na kuwasimamia kupitia: mapendeleo# faragha katika kipengele cha uthibitisho wa onion services.

Tor Browser 9.5 uthibitisho wa onion]


Kama wewe ni mtengenezaji programu, jifunze namn ya kulinda onion service zako kutumia uthibitisho wa mtumiaji.


Viashiria vya usalama vya URL vilivyoboreshwa

Usaidiaji wa zamani wa Browser kwenye tovuti hupitiswa kupitia mfumo salama wa usafirishaji ikiwa na alama ya kufuli ka kijani. Katikati ya mwaka 2019, alama ya kufuli ya kijani ya awali ilikuwa ya kijivu, iliyolenga kuwekea mkazo chaguo msingi (salama) hali ya muunganiko na isipokuwa kuweka mkazo zaidi kwenye muunganiko uliovunjika ua usio salama. Browser wakuu kama Firefox na Chrome walielewa kuwa ni faida kwa msingi mzima wa mtumiaji kama watakutana na uzoefu unaojulikana kwa watumiaji wote. Tunawafata Firefox katika maamuzi haya, na tumeboresha viashiria ya ulinzi vy Tor Browser ili kuwarahisishia watumiaji kuelewa pale wanapotembelea tovuti isiyo salama.

Tor Browser 9.5 Viashiria ya u=Usalama vya URL]

Kurasa zenye dosari kwenye onion services

Wakati mwingine watumiaji wanapata wakati mgumu kuzipata tovuti za onion. Katika toleo lilopita la Tor Browser, inapotokea tosari ya muunganiko katika onion service, watumiaji hupokea ujumbe wa dosari wa Firefox, bila taarifa kuhusu kwa nini wameshindwa kuunganisha na tovuti ya onion.

Katika toleo hili, tumeboresha namna kivinjari cha Tor kinavyowasiliana na watumiaji kuhusu huduma, wateja na dosari za upande wa mtandao ambazo zinaweza kutokea pale wanapojaribu kutembelea kwenye huduma ya onion. s]Sasa Tor Browser inaonesha mchoro rahisi wa muunganiko na inaonyesha wapi dosari imetokea. Tunataka jumbe hizi zieleweke na wapate taarifa bila ya kuelemewa.

Tor Browser 9.5 tovuti zenye dosari katika tovuti za onion]

Majina ya Onion

Kwa sababu ya ulinzi wa kriptographia, URLs za onion services sio rahisi kwa wanadamu kukumbuka (mfano https://torproject.org vs. http://expyuzz4wqqyqhjn.onion/). Hii inawapa ugumu watumiaji kugundua au kurudi katika tovuti ya onion. Tumegundua kuwa mwanzoni, watengenezaji programu walilikabili tatizo hili kwa njia tofauti, zaidi na suluhu kwa huduma zao. Ikizingatiwa kuwa hakuna suluhisho linalo fanya kazi kwa usahihi katika makundi yote ya watumiaji, pia tumelikabili tatizo hili kwa namna nyingi. Kwa toleo hili, tumeshirikiana na Freedom of Press Foundatio (FPF) na Electronic Frontier Foundation HTTPS Everywhere kutengeneza uhakiki wa kwanza wa dhana ya majina ya binadamu ya kukumbukwa kwa ajili ya usalama wa anwani za onion services:

Ukatizaji:
    theintercept.securedrop.tor.onion
    http://xpxduj55x2j27l2qytu2tcetykyfxbjbafin3x4i3ywddzphkbrd3jyd.onion
Lucy Parsons Labs:
    lucyparsonslabs.securedrop.tor.onion
    http://qn4qfeeslglmwxgb.onion

Freedom of Press Foundation imefikia namba ndogo ya vyombo vya habari vilivyoongezeka kwa ushiriki, na Tor pamoja na FPF wataungana kuzingatia hatua zinazofuata kwa kuzingatia mrejesho wa dhana ya uhakiki ya awali.

Tor Browser 9.5 Majina ya Onion]

toa maoni

Ikiwa una mapendekezo juu ya jinsi tunavyoweza kuboresha toleo hili, tafadhali tujulishe. Asante kwa timu zote katika Tor, na kwa wale wengi waliojitolea, ambao wamechangia kwa toleo hili.

Unaitaji msaada?

Angalia FAQ katika jamii yetu

Tembelea Msaada

Wasiliana

wasiliana na sisi moja kwa moja!

Jiunge nasi kwenye IRC